Wednesday, 3 May 2017

JUMLA YA WATOTO ISHIRINI WAWEKEWA MIKONO YA KIPAIMARA NA ASKOFU MKUU KANISA ANGLIKANA TANZANIA DR JACOB CHIMELEDYA


Jumla ya watoto ishirini(20) waliwekewa mikono na kupakwa mafuta katika Sacramenti ya ibada ya kipaimara iliyofanyika siku ya jumapaili Tarehe 30 Mwezi wa Nne katika kanisa la Anglikana kunduchi ambapo ibada hiyo ilishuhudiwa na zaidi ya waumini mia nne wakijitokeza kushuhudia uwekwaji mikono kwa vijana hao waliopata mafunzo kwa zaidi ya miezi Sita.

Ibada hiyo iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Tanzania Dr Jacob Chimeledya pamoja na Kasisi Kiongozi wa Dayosisi ya Dar es salaam Jerome Napela na Archidikini wa kinondoni pamoja padre wa Mtaa Rev Canon Mwanja katika ibada hiyo masomo ya siku hiyo yalisomwa na Vijana waliowekewa mikono na kupakwa mafuta ya Kipamaira 

Elizabeth Albert Malusu akisoma somo la kwanza ....

Akizungumza wakati wa Mahubiri Askofu mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania ambaye Pia ni Askofu mkuu wa Dayosisi ya Mpwapwa Dr Jacob Chimeledya

Amesema daraja ambalo watoto hao wamepata sio Daraja la kisherehe bali ni Daraja la kiroho na kuishi katika matendo ya kiimani ambayo yanamtukuza yesu kila siku, amesema kuwa wazazi wengi na watoto wengi mara baada ya kupata kipaimara basi mawazo yao uhamia kwenye Sherehe ambapo huko mara nyingi hatukuzwi kristo:- aliongeza kwa kusema Maisha ya kipaimara yamejijenga zaidi katika kuishi katika sara kila siku iendayo kwa Mungu Dr Chimeledya alitoa mfano kuwa Vitabu walivyokuwa navyo siku ya kipaimara ni silaha tosha na Muongozo Mzuri zaidi katika sara .

amewaasa kuwa katika Maisha ya sasa ambayo shetani ameeendelea kujidhirisha wazi wazi wanatakiwa kujibidiiisha zaidi katika Maisha ya kiroho kwani ulimwengu umebadilika sana tofauti ilivyokuwa miaka ya Nyuma ambapo kutoka na hali ya teknolojia shetani anajificha sana lakini anajiinua wazi wazi sana tofauti na ilivyokuwa Mwanzo kwa hiyo vijana na wazazi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuliko wakati Mwingine wowote kuhakikisha kanisa linasonga mbele.

Katika hatua Nyingine Baba Askofu Dr Jacob Chimeledya aligusia juu ya Ziara aliyoifanya Nchini Nigeria alikokuwa kabla hajafika katika kanisa la Anglikana kunduchi lililopo karibu na Shule ya Msingi Mtakuja kuwa alikwenda Nchini Nigeria ambako alikutana na maaskofu wenzie kuzungumzia Juuu ya kushuka Thamani juu ya Uuungu wa Yesu ambapo Nchini Nigeria unaonekana kushuka kwa hatua kubwa zaidi hasa kupanuka kwa Vitendo vya Ushoga.

amesema Vitendo vya Ushoga vinavyotoka katika nchi za Magharibi vimeharibu sana imani ya kikristo kiasi cha kuonekana kanisa halina maana mbele ya jamii, katika ziara hiyo ambayo amesema ilikuwa na lengo la kurejesha heshima na Uuungu wa Yesu kristo amesema kuwa Vitendo vya Ushoga katika kanisa havikubariki na vinaharibu kabisa heshima ya kanisa kwa sasa kwani vijana wengi wamekuwa wakiharibikiwa na wengine kuingia katika Dhambi ambazo laana zake ni kubwa sana .

Ibada hiyo ilianza na maandamano yaliyofanyika kutoka kanisa la zamani ambalo sasa linatumika kama Darasa la jumapili pia ilimalizika kwa maandamo kama ilivyoanza 
PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI YA KIPAIMARA HAPO CHINI

























Friday, 20 January 2017

UJENZI WA KANISA ANGLIKANA KUNDUCHI WAKATI LIKIWEKWA JAMVI

Chini ni mchoro wa ramani ambao utatumika katika ujenzi wa kanisa la st Michael kunduchi.
Chini Father Rev Richard kamenya akitafakari jambo na mwinjilisti Michael Ndawile okroro Father kwa kamenya kwa sasa amepata uhamisho na ansalisha kanisa la anglikana makuburi.

Chini ni wana kwaya wa kanisa la st Michael wakitazama ufundi wa upiga picha za video unaofanywa na Juma kazimoto.





Pichani ni mafundi wakifanya kazi ya kuweka jamvi katika kanisa la mtakatifu michael kunduchi mnamo mwaka elfu mbili na Nne ili kuhakikisha ndani ya miaka mitano ijayo wanasari katika kanisa hilo 


Hii ni moja kati uwajibikaji uliofanywa miaka ya nyuma katika kuhakikisha kuwa kazi ya Bwana inafanyika na inatimilika 

Moja kati ya mafundi wakimwaga zege ilikukamilisha moja kati ya hatua za kwanza za ujenzi wa kanisa

Mafundi wakianza kutemgeneza sehemu ya kusomea matangazo kule juu madhabauni janzi limeanza kukauka

HAYA NDIO MAENDELEO YA UJENZI WA KANISA ANGLIKANA KUNDUCHI !





 HII PICHA INAYONYESHA KANISA LA ANGLIKANA KUNDUCHI KARIBU KABISA NA SHULE YA MSINGI MTAKUJA KWA MBELE IKIONYESHA MAENDELEO YA UJENZI YANAVYONDELEA KUJENGA NYUMBA YA KUMSHUKURU .




HAPA NI MUONEKANO WA MBELE KWA JUU LIKIONYESHA MADHABAHU  ITAKAVYOKUWA IKIONEKANA .



MUONEKANO HUU NI WA PEMBENI WA KANISA HILI UKWELI NI KWAMBA WAMEDHAMILIA KUJENGA  HILI AMBALO LITAWEZA KUCHUKUA WAAMUNI ZAIDI YA MIA MOJA KWA MISA .


HII NI PICHA INAYOONYESHA KANISA HILI NYUMA JINSI LINAVYOJENGWA KWA USTADI WA 
HARI JUU MUNGU
 AWABARIKI SANA WANAOJENGA KANISA HILI.

HII NI MOJA KATI YA SEHEMU AMBAZO ZINARAJI KUMALIZIKA PUNDE MARA
 BAADHI YA MAMBO YA KAMATI YA UJENZI YATAKAPO KAMILIKA






















KURASA BADO IPO KATIKA MATENGENEZO